Notice: session_start(): Ignoring session_start() because a session is already active in /home/shbiamlu/public_html/btitz.org/app/helpers.php on line 3
Brand Tanzania Initiative
BTI Logo Brand Tanzania Initiative

Warning: include(/home/shbiamlu/public_html/btitz.org/mwandemange/includes/database.php): Failed to open stream: No such file or directory in /home/shbiamlu/public_html/btitz.org/views/public/news_single.php on line 5

Warning: include(): Failed opening '/home/shbiamlu/public_html/btitz.org/mwandemange/includes/database.php' for inclusion (include_path='.:/opt/alt/php82/usr/share/pear:/opt/alt/php82/usr/share/php:/usr/share/pear:/usr/share/php') in /home/shbiamlu/public_html/btitz.org/views/public/news_single.php on line 5

BTI TABORA YAPATIWA MAFUNZO

Published: April 21, 2026

UFUFUZI WA BTI TABORA WAANZA RASMI Tarehe 11 Aprili 2026, katika ukumbi wa Watermelon Hotel – Nzega, Mkoa wa Tabora, yalifanyika mafunzo ya awali ya Utaifa na Uzalendo yaliyowakutanisha wajumbe 15 kutoka Wilaya za Tabora, Igunga na Nzega. Kupitia mafunzo haya yaliyoongozwa na Mratibu wa BTI Kigoma, Ndugu Zamoyoni William Uzale, dhamira ya kufufua upya BTI Tabora imeanza kuonekana kwa vitendo. Baada ya mafunzo ya saa mbili yenye mjadala mpana na uelewa wa kina, wajumbe 12 walijitokeza kwa hiari na kukubali kuunda upya timu ya BTI Tabora—hatua inayofungua ukurasa mpya wa ujenzi wa Utaifa na Uzalendo katika mkoa huo. Hatua hii imeambatana na kuundwa kwa uongozi wa muda pamoja na mifumo ya mawasiliano itakayohakikisha BTI Tabora inakuwa hai, imara na yenye mwelekeo sahihi. Jitihada za Ndugu Zamoyoni Uzale zinaendelea kudhihirisha utekelezaji makini wa maelekezo ya KM kwa vitendo, na kuleta uhai mpya katika maeneo yaliyokuwa kimya. **BTI Tabora imerudi. Safari imeanza.** ?? Zamoyoni William Uzale Mratibu – BTI Tabora 16/04/2026 #BTITabora #Uzalendo #Utaifa #Leadership #Tanzania